Tuesday, 9 May 2017

MJUE MLINZI WA MAISHA YAKO KILA SIKU

Ukijaribu kutafakari sana, ni nani akupaye uzima kila iitwapo leo, na usalama maishani bila shaka ni Mungu tuu ndiye jibu la swali lako, na ndipo utakapogundua sasa kuwa Mungu anatupenda sana, maana kila siku tunaamka wazima, na tunashuhudia au kusikia kuwa watu wa mahali fulani, wengine wakiwa ni ndugu zetu wanatangulia mbele ya haki! lakini sisi tunaamka ni wazima na kuendelea na shughuli zetu mbalimbali kama vile kilimo, ufugaji, masomo, biashara, usafirishaji, ujenzi, na nyinginezo nyiingi kwa ujenzi wa familia zetu, maisha yetu na taifa letu kiujumla.
  • Kiukweli wakati tunayafanya yote haya, Mungu yu pamoja nasi na katika kila magumu na shida, mfano njaa, ukame, magonjwa, ajali, na kushindwa maishani Mungu anatuvusha na kutushindia maana yeye yu pamoja nasi kila mahali. Isa 41:10 inaeleza kuwa, "Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe, usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu".  Kutokana na neno hili, tunapata kuthibitisha kabisa kuwa Mungu yu pamoja nasi, na yuko tayari kututetea katika Mengi, tusiogope.
  • Cha msingi ni kumkumbuka Mungu katika nyakati zote, za shida na raha, na kuwa na imani tuu ya kuwa katika kila tukiombacho tutakipokea kiwe chetu (Mk 11:24).
  • Duniani ni mahali ambapo Ibilisi alitupwa kutoka Mbinguni (Ufu 12:9), kwa hiyo yupo hapa na anatenda kazi kila wakati (1Pet 5:8), lakini maombi pekee yanatufanya tumshinde, tukiomba bila kuchoka kwa imani, huku utakatifu ukitufunika (1pet 1:15-16). Si kwamba tuna nguvu sana za kumshinda shetani, ila Ulinzi wa Mungu kwetu na neema yake ndiyo hutushindia maana Mungu akiwa upande wetu ni nani aliye juu yetu? (Rum 8:31).
  • Roho mtakatifu aliye ndani yetu ndiye mkuu kuliko Ibilisi aliye duniani (1Yoh 4:4), hivyo yeye anatulinda na utendaji kazi wa Ibilisi Maishani mwetu, kwa hiyo tusiogope, maana tunaye mtetezi, mlinzi wa ajabu na cha msingi tuzidi kumkaribia kila iitwapo leo, maana kwa kufanya hivyo, shetani atakimbia, tukizidi kumpinga (Yak 4:7-8).
  • Amani ya BWANA iwe nawe mtumishi wa Mungu, maana yeye yu pamoja nasi kila wakati, kuwa mbali na Mungu ni kukosa ulinzi wa kutosha, na kuwa chini ya mikono ya Ibilisi! hivyo sogea sasa kwa Mungu wetu aliye hai kupitia njia kuu, ambaye ndiye Kristo Yesu, (Yoh 14:6, "Yesu akamwambia, mimi ndimi njia, na kweli, na uzima, mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi").
           PATA SASA WOKOVU UISHI KWA AMANI MAISHA YAKO YOTE, 
          HAPA DUNIANI NA MBINGUNI PIA.

No comments:

Post a Comment