Friday, 28 April 2017

KUOKOKA NI HAPA DUNIANI


 NA JACKSON, MWANDU MUYI
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza kuwa kuokoka ni nini hasa na ni kweli kunawezekana hapa duniani. Swali hili limewafanya wengine kutomwamini Bwana Yesu kuwa ni mwokozi wa maisha yao maana hawajui kuwa kuokoka ni hapa duniani, lakini ukweli ndio huo kwamba wokovu tunaupata hapa duniani.
"Kuokoka" ni  kumwamini Bwana Yesu kwa moyo wako  na kukiri kwa kinywa chako kuwa alikuja katika mwili na anao uwezo wa kukusamehe dhambi zako zote ulizotenda haijalishi ni kubwa kivipi, (Rum 10:9)na anaweza kukuokoa na taabu mbalimbali za hapa duniani, (Mt 11:28) na kukufikisha Mbinguni salama, maana alikuja ili tuwe na uzima wa milele (Yoh 3:16).
 Mk 16:16 inaeleza kuwa, "aaminiye na kubatizwa ataokoka, asiyeamini atahukumiwa". Hivyo hapa tunagundua kuwa ukimwamini Bwawna Yesu utakuwa umeokoka, hutahukumiwa tofauti na hapo utahukumiwa!
Mt 1:21 inaeleza utabiri wa kuzaliwa kwa Bwana Yesu, na kazi atakayoifanya hapa duniani, ("Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao") kama ilivyotabiriwa na Nabii Isaya (Isa 7:14).
Mdo 2:21 inaeleza kuwa, "Na kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa" ikimaanisha kwamba atakayemwita Bwana Yesu katika shida zake, na dhambi zake ataokolewa (ataokoka). mtu anaweza kumwita Bwana Yesu akiwa duniani kabla hajafa, akifa nafasi hiyo haipo tena! hivyo kuokoka ni hapa duniani.
Nyakati za Mitume wa Bwana Yesu, baada ya Yesu kupaa mbinguni, watu wengi walikuwa wakiokoka au wakiokolewa maana walimwamini Bwana Yesu kutokana na mahubiri na Mafundisho waliyopatiwa na mitume (Mdo 2:46-47), lakini si nyakati hizo tuu, hadi sasa Bwana Yesu anatenda kazi hiyo ya kuokoa watu waliopotea (wenye dhambi, walio upande wa adui shetani) na wenye shida.
Zab 16:3, "Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao". Hapa watu wanaotajwa ni watu waliookoka, waliopo hapa duniani, wanaoishi maisha ya kumpendeza Mungu na kujiepusha na uovu, hawa ndio Mungu aliopendezwa nao, hivyo kuokoka ni hapa duniani.
Mt 28:19-20 inatoa agizo kwa watu ambao tayari wameokoka kuwa wawafundishe na wengine waliopo ulimwenguni au duniani kuwa yawapasa nao wamwamini Bwana Yesu (waokoke), wabatizwe kwa maji mengi kwa Jina la Baba na la Mwana (Yesu) na Roho Mtakatifu na pia wayashike yote ambayo Bwana Yeseu aliwafundisha Mitume, au yote ambayo tuliookoka tumefundishwa na Watumishi wa Mungu wachungaji wetu ili kwamba nao wawe sawa nasi, tuwe wanafunzi wa Yesu sote, na huko ndiko kuokoka, kumwamini Bwana Yesu katika Yote na kufuata maagizo yake.
 Baada ya kuzaliwa tu Bwana Yeesu katika mji wa Bethlehemu, malaika wa BWANA waliwajia watu waliokuwa wakichunga mifugo yao na kuwaamnia kuwa, "maana leo katika mji wa Daudi  amezaliwa; kwa ajili yetu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana". (Lk 2:9-11). Neno "Mwokozi" lina maana ya "anayeweza kuokoa", au "anayewaokoa watu", au "anayefanya watu waokoke"; hivyo ukimwamini Bwana Yeesu kwa moyo wako na Kukiri kwa kinywa chako kuwa ni mwokozi wa maisha yako utaokoka, hapahapa duniani.
 Basi baada ya kuokoka,mtu  huanza kuishi maisha mapya katika ufalme mwingine mpya wa nuru (2Kor 5:17, Kol 1:13).
Najua sasa umefahamu kwa sehemu kuwa kuokoka ni hapa duniani, hivyo chukua uamzi sasa wa kufanya hivyo; kwa wewe mwenzangu ambaye tayari umeshaokoka au umeshampa Bwana Yesu maisha yako, basi tujitahidi kumtunza yeye maisha yetu yote, maana hatujakamilika bado, yeye ndiye mkamilishaji mkuu, na utimilifu wa wokovu wetu sasa ni pale tutakapohesabiwa haki na kupewa uzima wa milele, na kuishi naye Mwokozi wetu Mbinguni milele na milele (Mt 24:13, Ufu21:1-7).
MUNGU AKUBARIKI SANA USOMAYE UJUMBE HUU.

Thursday, 27 April 2017

UJUE UPENDO WA MUNGU KWAKO


Mbinguni ni pazuri sana, pana utukufu wa Mungu, na furaha ya ajabu hujapata ona!
 NA JACKSON, MWANDU MUYI

Uumbaji wa Mungu juu ya Binadamu, ni ishara mojawapo ya upendo wa Mungu kwetu, maana alikuwa na makusudi makubwa kwetu ya kwamba tumtumikie na tumwabudu yeye peke yake. Mungu alikuwa akiongea na wana wa Israeli wakati wakiwa safarini kwenda Kanaani, ambapo aliwaapia kuishi maisha yao mahali huko, nchi inayotoa asali na maziwa(Yenye baraka kuu za Mungu na ushindi daima), akiwaambia kuwa watamtumikia yeye, naye atakibarikia chakula chao, maji yao na kuwaondolea ugonjwa kati yao (Kut23:25). Katika (kut 20:1-6), Mungu aliwaambia juu ya ibada ambayo wanatakiwa kuifanya kuwa iwe ya kumwelekea yeye tuu, pasipo kuwa na Miungu mingine. Hapo makusudi makuu ya Mungu yaliyodhihirishwa kwa Mwanadamu ni kwamba anapaswa Kumwabudu Mungu na Kumtumikia maishani mwake, maana yeye anashughulika ns maisha yetu ya kula siku, na anatenda zaidi ya yale tuyawazayo na kuyaomba (Efe 3:20). Hapa tunagundua kwamba kila mambo tunayoyahitaji toka kwake, anao uwezo mkubwa wa kutupatia, na neno lakelinasema kuwa anajishughulisha sana na mambo yetu(1Pet 5:7).
Upendo wa Mungu ulionekana pia pale alipomtoa mwanaye wa pekee (Bwana Yesu, Mungu Mwana, Neno) ili aje ulimwenguni kutukomboa toka dhambini, mikononi mwa shetani, na Kutupa uzima wa Milele tukimwamini kiukweliukweli(Yoh 3:16). Ni jambo moja la ajabu ambalo wanadamu wengi huwa wanalishangaa, maana si kazi rahisi mtu kujitoa na kufa kwa ajili ya watu wengine, lakini kwa rehema zake Mungu jambo hili liliwezekana. Mwanadamu aliyekuwa na mizigo ya dhambi, yote ilikwisha Pale Bwana Yesu alipoangikwa msalabani. Kwa wale ambao bado hawajampa Yesu maisha yao ni vyema kumpa sasa, maaana Mwana wa Mungu alikufa msalabani kwa ajili yao (Isa 53:5), naye ndiye mwenye mamlaka ya Kusamehe (Mt 9:6), hivyo wasiwe na wasiwasi kabisa, haijalishi wametenda dhambi kubwaw kiasi gani, zinasamehewa zote, zinafanywa nyeupe kama theluji (Isa 1:18).
Huruma za Mungu, Rehema zake na Neema zake atoazo kwetu kila iitwawpo leo, ni ishara mojawapo ya kuwaw Mungu anatupenda sana. Hebu fikiria kidogo jii ya yafuatayo:
  • Pumzi yote tuipatayo kila siku inatoka wapi au kwa nani?
  • Ni nani atusafirishaye toka siku moja hadi nyingine tunaamka tu wazima kabisa?
  • Ni nani anayetushindia kila siku dhidi ya maadui wote wa kimwili na kiroho?
  • Ni nani atupaye mvua kila msimu wa kilimo na jua kila siku kwa manufaa yetu?
  • Tunapata wapi nguvu ya kuendelea mbele kila tunapopatwa na magumu maishani mwetu?
Bila shaka mtu yeyote ambaye "Ameokoka" au "Hajaokoka" atakuwa na jibu moja tuu ambalo ni MUNGU MUWEZA WA YOTE. Swali linakuja kwawmba kwa nini wewe ambaye hujaokoka bado unakuwa na moyo mgumu kumpa Yesu maisha yako, ili umwabudu Mungu katika roho na kweli maana anakutimizia mahitaji yako yote? Huu ndio upendo mkuu wa Mungu kwa watu wake, wema na wabaya. Itafika siku Mungu atachoka kuwavumilia kila watenda dhambi na wasiomwamini Bwana Yesu, na hapo ndipo watakapokuja kujuta kwa nini hawakuamua mapema kuokoa, maana ni kukiri tuu kuwa Bwana Yesu ni Bwana na Mwokozo wa Maisha Yao na kumwanini katika yote(Rum 10:9). Bwana Yesu amechelewa kuja tambua ili kuhakikisha kuwa kila mtu chini ya jua analisikia neno lake na anawavumilia wote ambao bado hawajaamua kumpa maisha yao maana hapendi wote wapotee, bali wote wafikilie toba (2Pet 3:9).
"MPE SASA YESU MAISHA YAKO NA UKUBALI KUONGOZWA NAYE ILI TUISHI KWA BARAKA HAPA DUNIANI NA KWA USHINDI ZAIDI, LAKINI PIA MBINGUNI KWAKE TUKAISHI MILELE KWA FURAHA ISIYO KIFANI"(Ufu 21:1-7).
 Kwa msaada zaidi wa Kimungu, piga 0768680106 au tembelea tovuti lubanajackson24@gmail.com
MUNGU AKUBARIKI SANA.

Wednesday, 26 April 2017

UKWELI KUHUSU UUNGU WA YESU: THE TRUTH THAT JESUS IS GOD.

Mara nyingi tumekuwa tukijiuliza ni kivipi Yesu ni Mungu, maana alizaliwa binadamu kama binadamu wengine. Kutokufahamu uungu wa Yesu kumewafanya watu wengi kutomwamini na kutompa maisha yao na kutomwabudu kabisa wakijua kuwa ni dhambi kumwabudu Bwana Yesu, maana ni Binadamu kama binadamu wengine.
Zifuatazo ni baaadhi ya sababu za Yesu kuitwa Mungu, na ndivyo alivyo milele na ukweli huu hautabatilika milele.
  1. Maandiko matakatifu yenyewe yanathibitisha hili. Mfano (a) Isa 9:6 "Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamumu; na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani" (b) Flp 2:5-7;  (5)"Iweni na nia iyo hiyo ndani yaenu ambayo pia ilikuwemo ndani ya Kristo Yesu (6) ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu,.............. (7)bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa na mfano wa mwanadamu". Pia waweza kusoma Mt 1:23, Yoh 1;1 na Lk 2:11.
  2. Alihusika katika uumbaji wa Binadamu na viumbe wengine. Yoh 1:3 "Vyote vilifanyika kwa huyo, wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika" Pia Mwa 1:26 "Mungu akasema, na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu............". Hapa Yesu, ambaye ni Mungu Mwana alishirikiana na Mungu Baba na Mungu Roho Mtakatifu (Utatu Mtakatifu; the God's Trinity) katika kumuumba mwanadamu.
  3. Alikuwepo tangu zamani, hata kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu. Yoh 8:56-58 "Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona akafurahi...........Yesu akawaambia, Amin amin nawaambia, Yeye ibrahimu asijakuwako, mimi niko". Hayo ni maneno ambayo Bwana yesu alikuwa akiwaambia Wayahudi, akiyathibitisha Mwenyewe kabisa.
  4. Kwa jina lake watu wengi walipona, na wanaendelea kupona, na kufanikiwa, na pia nguvu za giza zinawatoka, (Mdo 3:6, 8: 9-13 & 16:16-18) maana jina lake ni la kipekee, ambalo wanadamu tumepewa ili tuokolewe kwalo (Mdo 4:12). Pia yeye Mwenyewe aliponya watu wengi na kuwafungua mikononi mwa shetani.
  5. Manabii wa zamani na wazee walitabiri kuja kwake Bwana Yesu na kazi atakayoifanya hapa duniani, ambayo mwanadamu wa kawaida kuifanya ni vigumu, labda kwa uwezo wake Mungu. Mwa 49:10 "Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii". Pia Isa 11:1-10 inaeleza ujio wake Bwana Yesu, na jinsi atakavyokuwa akifanya kwa watu wote, wema na wabaya, kwa namna ya ajabu sana. Pia soma Kumb 18:15-19 & Isa 53: 3-5.
  6. Ana mamlaka ya Kusamehe dhambi kwa kila aliyetenda dhambi, akitubu kwelikweli. (Mt 9:6, Isa 53:5). Hakuna mwanadamu mwenye mamlaka hayo, na hatakuwepo.                                                                                                   Sasa nadhani umeshapata ufahamu juu ya uungu wa Yesu, rudisha sasa moyo wako kwake, ili umpe maisha yako siku zote; na wewe uliye naye imarisha uhusiano wako na yeye kupitia kumwabudu, kumwomba, kunyenyekea mbele zake, kujiepusha na dhambi na kumtegemea yeye peke yake maishani mwako, nawe utaona jinsi baraka zake zitakavyomiminika maishani mwako  hadi mwenyewe utashangaa maana zote hizi zipo kwa ajili yako siku zote, cha msingi, simama katika yeye, na kwa jinsi hiyo utamshinda mwovu ibilisi, mwizi wa baraka kwa mtu  ambaye hataki kusimama vizuri katika Mungu. Nakutakia wokovu mwema katika Kristo Yesu                             MUNGU AKUBARIKI SANA.

MWENYE DHAMBI HUNA RAHA

Fanya sasa maamzi  ya kuokoka na Bwana Yesu  yupo amekusubiria, anagonga mlango aingie moyoni mwako, mkubalie, usimhuzunishe, mkaribishe, anakupenda, anakubembeleza, anakuhurumia, hadi akakufia msalabani! mhurumie na wewe kama alivyokuhurumia, maana alikuja duniani kwa ajili ya dhambi zako, magonjwa yako, mateso ya kila namna uliyonayo, na pia kukuandaa kwa ajili ya kwenda kuishi naye Mbinguni, mahali pazuri sana alipopaandaa kwa ajili yako na kwa ajili yangu pia (Yoh 3:16,  Mt 11:28 & Ufu 21:1-7); MIMI NINAYE YESU, WEWE JE?

MAZINGIRA YA MBINGUNI

Ukiitazama video hii, unaguswa sana kujikaza kufika Mbinguni mpendwa, Tujitahidi tufike mahali ambapo BWANA ametuandalia, hapa Duniani sisi tu wapitaji tuu, wenyeji wetu upo Mbinguni.

Tuesday, 25 April 2017

SALVATION IS NEAR TO YOU WHEREVER YOU ARE.

Romans 10:9-10.
 9, "Because, if you confess with your own lips that Jesus is Lord and believe in your heart that God raised him from the dead , you will be saved".
10,  "For man believes with his heart and so is justified, and he co fesses with his lips and so is saved".
These two verses talk about the decision the person can take after hearing the Word of God, probably being preached in the church, Evangelical conferences, Worship Joint Masses, Easter conferences or Praise and worship sessions as well as door-to-door preaching programs, among others.
The decision the person has to take is either confessing that the Lord Jesus Christ is his or her Savior in the sin he or she possessed, the problems he faced or facing in the daily life, as well as in the Enemies that emerge in his or her life, both Spiritual and Physical enemies, or staying as he or she was at the beginning.
Most of the time the people have been hearing the Word of God, but they hardly take action of agreeing with it and allowing it to operate in their hearts. Normally, the Word of God is powerful, even if the people find it difficult to confess by their lips and believe by their hearts that Jesus is the Savior of their lives, this Word always talks within their heart and perhaps cause pains in them due to the actions they do in their lives. These actions includes Alcoholism, Adultery or illegal sexual practices, Telling the liar information, Killing other people for the sake of their own benefits, worshiping other gods, corruption and other actions which they think that they are getting benefits from them.
It is very dangerous to hear the World of God and give it up or leaving it unconsidered it in their lives.This is because, they are denying the voice of God and thus at any time they die, the action which comes spontaneously and abruptly, they will be cast in the Lake of burning Sulfur or Fire, where the Satan with its servants are going to be thrown! This is because their names will not appear in the Book of life (Revelation 20:15), since any person after receiving Jesus Christ as his or her Savior, his or her name is written in the Book of life.
"Receive the Lord Jesus Christ today so as to live forever the most enjoyable life in the Heaven as there are another life after death"
GOD BLESS YOU ALL.

Saturday, 22 April 2017

MAFANIKIO MAISHANI NI MIPANGO YA MAPEMA

THE UNIVERSITY OF DODOMA
Maisha ya dunia ya leo yana changamoto mbalimbali ambazo huwafanya watu wafanye maamzi mabaya ambayo huja kuwagharimu sana maishani mwao na kujutia walichoamua kukifanya mwanzoni, japo ni vigumu kubadilisha maana tayari maji yalishamwagika!

Kwa mfano, kuhusu mke wa kuoa, kijana asipopanga vizuri, atajikuta ameoa mke ambaye atatamani kuachana naye baada ya miaka fulani ya ndoa, japo sasa inakuwa haiwezekani, na akilazimisha, maisha tayari yamevurugika, watoto wanakosa pa kukaa, maana familia ikivunjika mzigo wa watoto ni kazi kuubeba, hivyo huenda mmoja wao akalemewa na huu mzigo, na mwingine kuukataa kabisa, na endapo wote wataukataa huu mzigo, basi watoto wanakosa kabisa pa kukaa, wanakuwa tena si wa baba au mama, bali wa MITAANI! jambo linaloumiza sana maisha yao. Maisha hayapo duniani tuu, na mbinguni pia yapo, wazazi wakiwaacha watoto wakateseka ovyo, hukumu ipo juu yao, maana siku ya hukumu watoto watawahukumu wazazi wao kwa kuwatenda mabaya hayo, kwa sababu tuu hawakupanga sawasawa na kuamua kiukweliukweli kabla ya kuoana.