Wednesday, 26 April 2017

UKWELI KUHUSU UUNGU WA YESU: THE TRUTH THAT JESUS IS GOD.

Mara nyingi tumekuwa tukijiuliza ni kivipi Yesu ni Mungu, maana alizaliwa binadamu kama binadamu wengine. Kutokufahamu uungu wa Yesu kumewafanya watu wengi kutomwamini na kutompa maisha yao na kutomwabudu kabisa wakijua kuwa ni dhambi kumwabudu Bwana Yesu, maana ni Binadamu kama binadamu wengine.
Zifuatazo ni baaadhi ya sababu za Yesu kuitwa Mungu, na ndivyo alivyo milele na ukweli huu hautabatilika milele.
  1. Maandiko matakatifu yenyewe yanathibitisha hili. Mfano (a) Isa 9:6 "Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamumu; na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani" (b) Flp 2:5-7;  (5)"Iweni na nia iyo hiyo ndani yaenu ambayo pia ilikuwemo ndani ya Kristo Yesu (6) ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu,.............. (7)bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa na mfano wa mwanadamu". Pia waweza kusoma Mt 1:23, Yoh 1;1 na Lk 2:11.
  2. Alihusika katika uumbaji wa Binadamu na viumbe wengine. Yoh 1:3 "Vyote vilifanyika kwa huyo, wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika" Pia Mwa 1:26 "Mungu akasema, na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu............". Hapa Yesu, ambaye ni Mungu Mwana alishirikiana na Mungu Baba na Mungu Roho Mtakatifu (Utatu Mtakatifu; the God's Trinity) katika kumuumba mwanadamu.
  3. Alikuwepo tangu zamani, hata kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu. Yoh 8:56-58 "Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona akafurahi...........Yesu akawaambia, Amin amin nawaambia, Yeye ibrahimu asijakuwako, mimi niko". Hayo ni maneno ambayo Bwana yesu alikuwa akiwaambia Wayahudi, akiyathibitisha Mwenyewe kabisa.
  4. Kwa jina lake watu wengi walipona, na wanaendelea kupona, na kufanikiwa, na pia nguvu za giza zinawatoka, (Mdo 3:6, 8: 9-13 & 16:16-18) maana jina lake ni la kipekee, ambalo wanadamu tumepewa ili tuokolewe kwalo (Mdo 4:12). Pia yeye Mwenyewe aliponya watu wengi na kuwafungua mikononi mwa shetani.
  5. Manabii wa zamani na wazee walitabiri kuja kwake Bwana Yesu na kazi atakayoifanya hapa duniani, ambayo mwanadamu wa kawaida kuifanya ni vigumu, labda kwa uwezo wake Mungu. Mwa 49:10 "Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii". Pia Isa 11:1-10 inaeleza ujio wake Bwana Yesu, na jinsi atakavyokuwa akifanya kwa watu wote, wema na wabaya, kwa namna ya ajabu sana. Pia soma Kumb 18:15-19 & Isa 53: 3-5.
  6. Ana mamlaka ya Kusamehe dhambi kwa kila aliyetenda dhambi, akitubu kwelikweli. (Mt 9:6, Isa 53:5). Hakuna mwanadamu mwenye mamlaka hayo, na hatakuwepo.                                                                                                   Sasa nadhani umeshapata ufahamu juu ya uungu wa Yesu, rudisha sasa moyo wako kwake, ili umpe maisha yako siku zote; na wewe uliye naye imarisha uhusiano wako na yeye kupitia kumwabudu, kumwomba, kunyenyekea mbele zake, kujiepusha na dhambi na kumtegemea yeye peke yake maishani mwako, nawe utaona jinsi baraka zake zitakavyomiminika maishani mwako  hadi mwenyewe utashangaa maana zote hizi zipo kwa ajili yako siku zote, cha msingi, simama katika yeye, na kwa jinsi hiyo utamshinda mwovu ibilisi, mwizi wa baraka kwa mtu  ambaye hataki kusimama vizuri katika Mungu. Nakutakia wokovu mwema katika Kristo Yesu                             MUNGU AKUBARIKI SANA.

No comments:

Post a Comment