 |
| THE UNIVERSITY OF DODOMA |
|
Maisha ya dunia ya leo yana changamoto mbalimbali ambazo huwafanya watu wafanye maamzi mabaya ambayo huja kuwagharimu sana maishani mwao na kujutia walichoamua kukifanya mwanzoni, japo ni vigumu kubadilisha maana tayari maji yalishamwagika!
Kwa mfano, kuhusu mke wa kuoa, kijana asipopanga vizuri, atajikuta ameoa mke ambaye atatamani kuachana naye baada ya miaka fulani ya ndoa, japo sasa inakuwa haiwezekani, na akilazimisha, maisha tayari yamevurugika, watoto wanakosa pa kukaa, maana familia ikivunjika mzigo wa watoto ni kazi kuubeba, hivyo huenda mmoja wao akalemewa na huu mzigo, na mwingine kuukataa kabisa, na endapo wote wataukataa huu mzigo, basi watoto wanakosa kabisa pa kukaa, wanakuwa tena si wa baba au mama, bali wa MITAANI! jambo linaloumiza sana maisha yao. Maisha hayapo duniani tuu, na mbinguni pia yapo, wazazi wakiwaacha watoto wakateseka ovyo, hukumu ipo juu yao, maana siku ya hukumu watoto watawahukumu wazazi wao kwa kuwatenda mabaya hayo, kwa sababu tuu hawakupanga sawasawa na kuamua kiukweliukweli kabla ya kuoana.
No comments:
Post a Comment