![]() |
| Mbinguni ni pazuri sana, pana utukufu wa Mungu, na furaha ya ajabu hujapata ona! |
NA JACKSON, MWANDU MUYI
Uumbaji wa Mungu juu ya Binadamu, ni ishara mojawapo ya upendo wa Mungu kwetu, maana alikuwa na makusudi makubwa kwetu ya kwamba tumtumikie na tumwabudu yeye peke yake. Mungu alikuwa akiongea na wana wa Israeli wakati wakiwa safarini kwenda Kanaani, ambapo aliwaapia kuishi maisha yao mahali huko, nchi inayotoa asali na maziwa(Yenye baraka kuu za Mungu na ushindi daima), akiwaambia kuwa watamtumikia yeye, naye atakibarikia chakula chao, maji yao na kuwaondolea ugonjwa kati yao (Kut23:25). Katika (kut 20:1-6), Mungu aliwaambia juu ya ibada ambayo wanatakiwa kuifanya kuwa iwe ya kumwelekea yeye tuu, pasipo kuwa na Miungu mingine. Hapo makusudi makuu ya Mungu yaliyodhihirishwa kwa Mwanadamu ni kwamba anapaswa Kumwabudu Mungu na Kumtumikia maishani mwake, maana yeye anashughulika ns maisha yetu ya kula siku, na anatenda zaidi ya yale tuyawazayo na kuyaomba (Efe 3:20). Hapa tunagundua kwamba kila mambo tunayoyahitaji toka kwake, anao uwezo mkubwa wa kutupatia, na neno lakelinasema kuwa anajishughulisha sana na mambo yetu(1Pet 5:7).
Upendo wa Mungu ulionekana pia pale alipomtoa mwanaye wa pekee (Bwana Yesu, Mungu Mwana, Neno) ili aje ulimwenguni kutukomboa toka dhambini, mikononi mwa shetani, na Kutupa uzima wa Milele tukimwamini kiukweliukweli(Yoh 3:16). Ni jambo moja la ajabu ambalo wanadamu wengi huwa wanalishangaa, maana si kazi rahisi mtu kujitoa na kufa kwa ajili ya watu wengine, lakini kwa rehema zake Mungu jambo hili liliwezekana. Mwanadamu aliyekuwa na mizigo ya dhambi, yote ilikwisha Pale Bwana Yesu alipoangikwa msalabani. Kwa wale ambao bado hawajampa Yesu maisha yao ni vyema kumpa sasa, maaana Mwana wa Mungu alikufa msalabani kwa ajili yao (Isa 53:5), naye ndiye mwenye mamlaka ya Kusamehe (Mt 9:6), hivyo wasiwe na wasiwasi kabisa, haijalishi wametenda dhambi kubwaw kiasi gani, zinasamehewa zote, zinafanywa nyeupe kama theluji (Isa 1:18).
Huruma za Mungu, Rehema zake na Neema zake atoazo kwetu kila iitwawpo leo, ni ishara mojawapo ya kuwaw Mungu anatupenda sana. Hebu fikiria kidogo jii ya yafuatayo:
- Pumzi yote tuipatayo kila siku inatoka wapi au kwa nani?
- Ni nani atusafirishaye toka siku moja hadi nyingine tunaamka tu wazima kabisa?
- Ni nani anayetushindia kila siku dhidi ya maadui wote wa kimwili na kiroho?
- Ni nani atupaye mvua kila msimu wa kilimo na jua kila siku kwa manufaa yetu?
- Tunapata wapi nguvu ya kuendelea mbele kila tunapopatwa na magumu maishani mwetu?
"MPE SASA YESU MAISHA YAKO NA UKUBALI KUONGOZWA NAYE ILI TUISHI KWA BARAKA HAPA DUNIANI NA KWA USHINDI ZAIDI, LAKINI PIA MBINGUNI KWAKE TUKAISHI MILELE KWA FURAHA ISIYO KIFANI"(Ufu 21:1-7).
Kwa msaada zaidi wa Kimungu, piga 0768680106 au tembelea tovuti lubanajackson24@gmail.com
MUNGU AKUBARIKI SANA.

Ni kweli kabisa mtumishi wa Mungu, pasipo Yesu, Maisha ni ya kubangaiza!
ReplyDelete